March 26, 2013

DIY KITENGE BOW TIE


 Za kitenge hizo kutoka Kibua Designs
Umeipenda ipi?
Tiririka

***

Labels: , , , , ,

March 09, 2013

BATIK SHIRT DRESS

CLICK HERE TO SEE MORE >>>>

Labels: , , ,

March 08, 2013

HAPPY WOMEN'S DAY

Habari!

Naongea na wewe mwanamke mwenzangu
Hivi unajitambua?
Jipende, jithamini, jilinde, jikubali
Kuwa na msimamo na siku zote kuwa na uthubutu
Mwanamke sio chombo cha starehe kama wengine wanavyodhani
Mwanamke ni ua(flower),  mwanamke ni mlezi, hebu jithamini 

Wanawake na maendeleo, hebu tuache kukaa tu nyumbani, tujishughulishe ili tuweze kujikwamua kiuchumi, tuweze kulea familia zetu bila shida, tuepukane na utegemezi ili tusije itwa majina yasiyopendeza kama magolikipa.
Mwanamke wa sasa elimu, wenyewe tunasema education is sex
na tuamke basi, tunapopata fursa tuzitumie vizuri, ipasavyo
Tusitoe mwanya kwa yeyote kutuonea au kutukandamiza kwa sababu tu sisi ni wanawake. 
Tuungane tuwe wamoja ili tuliendeleze taifa letu kwani na sisi tuna mchango mkubwa sana katika ujenzi wa taifa hili

Wanawake tunaweza, tusisubiri kuwezeshwa, wenyewe tunaweza bila kuwezeshwa na mtu yeyote
Tuwe wajasiri, mwisho wa siku tutakuwa washindi
Tupendane, tusichukiane wenyewe kwa wenyewe na kuoneana wivu.
Tuwe na wivu wa maendeleo. Mwenzio akifanikiwa mfuate akupe maarifa na sio kumchukia bila sababu, kwa kufanya hivyo utajirudisha nyuma kimaendeleo wewe mwenyewe

Tuamke, tupambane

Wanawake oyeeeeeeeeee

HAPPY WOMEN'S DAY

xoxo

Kibua V

***

Labels:

March 06, 2013

DIY KITENGE NECKTIE
 Niaje wadau wangu? Mko poa?

Leo napenda kuwaletea  necktie ya kitenge(African print necktie)
Nimetumia kitenge cha wax kuitengeneza.
Ni rahisi sana hata wewe hapo home unaweza tengeneza yako kwa kutumia sindano ya mkono si lazima uwe na mashine ndio uweze tengeneza hii kitu.

Tai sio lazima itengenezwe kwa kitambaa laini, au lazima kitambaa kilichotoka ng'ambo. Kitenge pia kinaweza fanya maajabu. Wakati mwingine waweza tumia hata kanga.

Naahidi katika posts zangu zitakazofuata, nitaandaa post maalum ambayo itatoa somo namna ya kutengeneza necktie ya kitenge

Hayo tu ndio niliyonayo wadau wangu
Nawapenda sana

xoxo

***

Labels: , , , , ,